Jumatano 4 Novemba 2026 - 23:09
Ayatullah Al-Udhma Wahid Khorasani Alazwa Hospitalini/ Hali Yake kwa Ujumla ni Nzuri

Hawza/ Mmoja wa wajumbe wa ofisi ya Ayatullah Wahid Khorasani amethibitisha taarifa za kulazwa kwake hospitalini na kueleza kuwa, Alhamdulillah, hali yake ya kiafya kwa ujumla inaendelea kuwa nzuri.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Al-Haj Sheikh Hussein Wahid Khorasani, ambaye ni miongoni mwa Maraji' wakubwa wa Taqalidi, amelazwa katika mojawapo ya hospitali za mjini Tehran kwa ajili ya kufanyiwa baadhi ya taratibu za matibabu. Mchakato wa matibabu yake unaendelea chini ya uangalizi wa madaktari wanaomhudumia.

Mmoja wa wajumbe wa ofisi yake, alipothibitisha taarifa hizo, alimweleza mwandishi wetu wa habari kwamba, Alhamdulillah, hali ya kiafya ya Marji' huyu mkubwa wa Taqalidi kwa ujumla inaendelea kuwa nzuri.

Taarifa zaidi zitatolewa baadaye kadiri zitakavyopatikana...

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha